Wanajeshi wanaume na wanawake wa jeshi la akiba, simba wetu wa kiume na wa kike,

Nyuma ya kila mmoja wenu kuna nyumba inayowamisi. Watoto wanaongojea kukumbatiwa, wenzi wanaobeba mzigo, wazazi wanaohangaika. Kuna biashara mliyoijenga kwa mikono yenu wenyewe, masomo yaliyokatizwa na mipango iliyoahirishwa. Na katikati ya yote hayo, mnajitokeza, tena na tena, ili kuilinda Nchi ya Israel.

Nataka kuwaambia kutoka sakafu ya moyo wangu: Ahsanteni. Kwa ushujaa, kwa kujitolea, kwa ushirika na kwa kuipenda nchi. Mnatupa sisi sote usalama, na kwa uthabiti wenu mnalipatia taifa la Israel matumaini pia.

Kama Waziri Mkuu, wajibu wangu ni kuhakikisha kuwa nchi inasimama upande wenu na upande wa familia zenu. Shukrani zetu lazima zidhihirike katika maamuzi, katika bajeti na katika msaada unaoonekana katika maisha halisi yenyewe.

Kwa hivyo tumesukuma mbele ufadhili kamili wa ada ya masomo ya chuo kikuu kwa ajili ya shahada ya kwanza kwa wapiganaji wanaume na wanawake wanaostahili ndani ya mfumo wa “Mamadim LeLimudim”.

Tumesukuma mbele pointi za punguzo la kodi kwa wapiganaji wa akiba, ili kuacha fedha zaidi katika mapato halisi, na tukapanua kipaumbele kwa wanajeshi wa akiba katika mipango ya makazi na ugawaji wa viwanja.

Tumetenga mabilioni ya shekeli kwa ajili ya mipango ya msaada, malipo na ruzuku: kwa matumizi binafsi, uchumi wa kaya, kwa familia na kwa wanaotumikia vipindi virefu. Sambamba na haya, tumesukuma mbele msaada kwa watu waliojiajiri ambao biashara zao ziliathirika, msaada kufuatia kupoteza mapato katika familia na utatuzi kwa wanafunzi waliohitajika kuondoka katika viti vya masomo na kujitokeza kwenye utumishi.

Familia nzima pia inahitaji msaada. Kwa hivyo tumepanua huduma za kushiriki katika gharama za ulezi wa watoto na kambi za likizo za watoto, msaada wa kuhama makazi, matibabu ya kisaikolojia na ya wanandoa, na vocha za likizo, kulingana na vigezo vya ustahiki.

Tumesukuma mbele pia ulinzi wa ajira kwa wenzi wa wanajeshi wa akiba, na marejesho ya safari katika Barabara Kuu ya 6 wakati wa kuelekea kwenye utumishi na kurudi kutoka huko. Ninawashukuru wenzangu serikalini na katika Bunge la Israel (Knesset), akiwemo Mwenyekiti wa Muungano Ofir Katz, kwa ushirikiano katika kusukuma mbele sheria na misaada.

Ninajua kwamba hata baada ya hatua hizi zote kuna matatizo yanayohitaji utatuzi. Wajibu wetu unaendelea hata siku inayofuata baada ya kurejea nyumbani.

Na kwa wake za wanajeshi wa akiba, kwa wenzi, kwa watoto na kwa wazazi: Ahsanteni kwa nguvu mnazowapa wapendwa wenu. Kwa usiku za mahangaiko, kwa kuendesha nyumba na kwa nyakati nyingi sana ambazo mnatakiwa kuwa imara. Kujitolea kwenu ni sehemu isiyotenganishwa na usalama wa Israel.

Wanajeshi wetu wa akiba wapendwa, ninyi ni simba. Ninajivunia nanyi, ninawapenda na ninawashukuru kwa niaba ya taifa lote la Israel. Tutaendelea kuchukua hatua ili muweze kuilinda nchi, kujenga mustakabali wenu na kurudi kwa familia zenu mkiwa mmeinua vichwa juu. 🇮🇱